Skip to main content
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa awataka wakaazi wa Lindi kulima zao la alizeti kwa wingi

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa amewataka wakazi wa mkoa wa Lindi kulima zao la alizeti kwa wingi baada ya serikali kupata mwekezaji wa kununua zao hilo na kwa bei nzuri.

Ametoa mwito huo wakati akizungumza na wananchi wa vijiji mbalimbali vya wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi ambako amepita kuwasalimia wananchi wa jimbo lake na kuhimiza kazi za maendeleo akiwa katika siku nne za mapumziko ya mwisho wa mwaka

Amesema mwekezaji huyo atawapatia mbegu ambapo kila ekari moja mkulima atapata kilo tano, na akivuna zao hilo kila ekari atapata magunia 20 na kila gunia lina uwezo wa kutoa lita 20 za mafuta 

Bei ya dumu moja la lita 20 ni shilingi elfu sitini kwa hiyo katika ekari moja mkulima ana uhakika wa kupata shilingi milioni 1.2.

 

 

 

Hata hivyo amemwagiza mkuu wa idara ya kilimo (umwagiliaji na ushirika) wa wilaya hiyo, Violeth Byanjweli  afanye kazi ya kuratibu ni wakazi wangapi wana mashamba ya alizeti na wangapi wako tayari kuanzisha kilimo hicho ili mbegu zitakapopelekwa  iwe rahisi kuwasambazia  kwa wakulima

 

Add new comment

Plain text

  • No HTML tags allowed.
  • Lines and paragraphs break automatically.
  • Web page addresses and email addresses turn into links automatically.