Skip to main content
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa azitaka kila tarafa kupandisha hadhi kwa baadhi ya shule kwa kuweka miundombinu sawa

Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa amesema serikali haitavumilia kuona mamia ya vijana waliofaulu mitihani ya darasa la saba na kuchaguliwa kuingia kidato cha kwanza wanabaki nyumbani kutokana na uhaba wa madarasa.

 

Ametoa  kauli hiyo wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa mkoa wa lindi Mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa huo kwenye ikulu ndogo wilayani Nachingwea.

 

Amesema serikali ya awamu ya tano imedhamiria kutoa elimu ya bure kwa kila mtoto atashangaa kuona watoto wengine wanafaulu na wanashindwa kujiunga na elimu ya sekondari.

 

Amewataka wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri ambazo zimefaulisha wanafunzi lakini hazina madarasa na madawati ya kutosha kujipanga upya ili kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu wanapata nafasi ya kuingia kidato cha kwanza

 

Amezitaka kila tarafa kuwa na sekondari moja ya kidato cha tano na sita, nakupandishwa hadhi kwa baadhi ya shule kwa kuweka  miundombinu inayotakiwa ya bwalo, jiko, mabweni, mifumo ya maji, madarasa na vyoo vya kutosha

 

 

 

Add new comment

Plain text

  • No HTML tags allowed.
  • Lines and paragraphs break automatically.
  • Web page addresses and email addresses turn into links automatically.