Skip to main content
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wajumbe wa baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) wakutane na wamiliki wa taasisi za kifedha ili kuangalia uwezekano wa kutoa mikopo yenye gharama nafuu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wajumbe wa baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) wakutane na wamiliki wa taasisi za kifedha ili kuangalia uwezekano wa kutoa mikopo yenye gharama nafuu.

Ametoa kauli hiyo leo alipokutana na wajumbe wa baraza hilo katika makazi ya waziri mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam.

Waziri mkuu amesema kuwa ni vema wajumbe hao wakakutana na wamiliki wa taasisi hizo ili kuwasaidia wananchi kupata mikopo yenye masharti nafuu itakayoza uchumi wao.

Awali mwenyekiti wa baraza hilo, Dokta John Jingu amesema kuwa baraza limezinduliwa Januari 8, mwaka huu na kukubaliana kuanza kazi katika maeneo yenye tija kwa wananchi ambayo ni kilimo, sanaa, ufugaji na uvuvi.

Amesema kuwa uwezeshaji katika maeneo hayo utaleta matokeo ya haraka kwa wananchi wengi kwa kuwa shughuli zao nyingi zimejikita katika maeneo hayo.

 

Add new comment

Plain text

  • No HTML tags allowed.
  • Lines and paragraphs break automatically.
  • Web page addresses and email addresses turn into links automatically.