Skip to main content
Wagonjwa wakiwa katika moja ya siptali humu nchini

Watu wawili wafariki na wengine 30 kulazwa kutokana na kulipuka kwa ugonjwa wa kipindupindu Singida

Watu wawili wamefariki na wengine 30 wamelazwa kwenye vituo mbalimbali vya afya vya halmashauri ya wilaya ya Singida kwa ajili ya matibabu, tangu ugonjwa wa kipindupindu uanze kulipuka Novemba 26, mwaka huu.

Mkuu wa wilaya ya Singida Elias Tarimo amesema kuwa ugonjwa huo umebainika kulipuka katika vijiji vya Merya na Msange, tangu mwezi uliopita, lakini mamlaka zimekifanya kuwa siri

Amesema kuwa kuchelewa kutolewa kwa taarifa hizo,  ni moja ya mambo yaliyochangia  ugonjwa huo kutodhibitiwa haraka hadi kusambaa katika maeneo mengine na kusababisha vifo vya  watu wawili na idadi wa wagonjwa waliougua  kuongezeka

Hata hivyo baada ya taarifa kutolewa na watu kuanza kuchukua hatua za kujikinga idadi wa wagonjwa imekuwa ikipungua siku hadi siku ambapo hivyo sasa wamebaki watu watano waliolazwa kwenye kambi ya Merya na Msange

Ametoa wito kwa wananchi kudumisha usafi wa mazingira, matumizi vyoo bora na kuchemsha maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kuzingatia kanuni nyingine zote muhimu za afya ili kuzuia mlipuko zaidi.

 

Add new comment

Plain text

  • No HTML tags allowed.
  • Lines and paragraphs break automatically.
  • Web page addresses and email addresses turn into links automatically.