Skip to main content
Mkuu wa Mkoa wa lindi Godfrey Zambi

Wananchi wa Jimbo la Ruangwa wapewa wiki mbili kuhakikisha wanajenga vyoo kujiepusha na Kipindupindu

Wananchi wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi wamepewa wiki mbili kuhakikisha kuwa wanajenga vyoo ili kujiepusha na ugonjwa wa kipindupindu.

 

Mwito huo umetolewa na mkuu wa mkoa huo, Godfrey Zambi kwa mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Joseph Mkirikiti kuwa afanye msako wa nyumba kwa nyumba ifikapo januari 15 mwakani na awatoze faini watakaoshindwa kujenga vyoo vya kisasa

 

Agizo hilo amelitoa jana wakati akizungumza na wananchi wa vijiji vya Namilema, Mbuyuni, Nandandara, Namkonjera, Muhuru, Chikundi na Chibula kabla ya kumkaribisha waziri mkuu kuzungumza na wakazi wa vijiji hivyo.

 

Waziri mkuu yuko Ruangwa kwa siku nne kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka na ameamua kutumia muda huo kuwasalimia wananchi wa jimbo lake na kuhimiza kazi za maendeleo.

 

Mkuu huyo wa mkoa amesema wakulima wengi wamevuna korosho msimu na baadhi yao wamelipwa vizuri, hivyo hawana budi kutumia sehemu ya fedha hizo kujenga vyoo ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko na hasa kipindupindu.

 

Add new comment

Plain text

  • No HTML tags allowed.
  • Lines and paragraphs break automatically.
  • Web page addresses and email addresses turn into links automatically.