Skip to main content
Meneja wa Upimaji, Wakala wa Vipimo, Richard Kadege, akiwaonesha waandishi kifaa cha kutunzia kumbukumbu za upimaji wa magari

Wakala va vipimo nchini kuweka stika katika mizani zote ili kudhibiti udanganyifu

Wakala wa vipimo nchini wanatarajiwa kuweka stika katika mizani zote zilizohakikiwa na mamlaka hiyo nchi nzima ili kudhibiti udanganyifu wa wafanyabiashara wasio waaminifu wanaowaibia walaji kupitia mizani,

Kaimu Mkurugenzi huduma za ufundi wakala wa vipimo Stellah Kahwa amesema ubora wa stika hizo hauwezi kughushiwa na kuendelea kuwapa nafasi nzuri walaji.

Uwekaji wa stika hizo maalum utaanza rasmi mapema mwakani, ikiwa ni njia mojawapo ya kwenda na teknolojia ya kisasa ya kuhakikisha mteja analindwa kwa kununua bidhaa inayoendana na kiwango cha fedha aliyotoa.

Naye kaimu meneja wa mawasiliano Irene John amesema stika hizo maalum zitawawezesha wanunuzi wa bidhaa kutambua vipimo halali vya bidhaa wanazonunua.

Miongoni mwa makundi yanayoathiriwa na matumizi mabaya ya mizani na vipimo ni pamoja na wakulima na hivyo kubuniwa kwa stika hizo kutawawezesha  kupata faida zaidi

 

Add new comment

Plain text

  • No HTML tags allowed.
  • Lines and paragraphs break automatically.
  • Web page addresses and email addresses turn into links automatically.