Skip to main content
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe

Wafanyibiashara wa Tanzania bara na visiwani washauriwa kuwa na ushurikiano

Wafanyabiashara wa Tanzania bara na visiwani wameshauriwa kuwa na ushirikiano wa kiabiashara ikiwemo  kubadilishana ujuzi ili kuendelea kuimarisha na kudumisha muungano.

Waziri wa elimu na mafunzo ya amali Riziki Pembe ametoa rai hiyo wilaya ya Maswa mkoani Simiyu alipokuwa akiingia makubaliano na kiwanda cha kutengeneza chaki cha Maswa.

Kufuatia makubaliano hayo kupitia wizara ya elimu na mafunzo ya amali vijana wake watapata mafunzo ya namna ya kutengeneza chaki kutoka kiwandani hapo

Kuwepo kwa ushirikiano  huo hususani kwa vijana wa pande mbili za muungano kutachangia kufikiwa kwa malengo ya kuwa na tanzania yenye viwanda na uchumi wa ifikapo 2025.

Mkuu wa mkoa huo Anthony Mtaka amempongeza rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dokta Ali Mohamed Shein kwa kutimiza ahadi yake ya kuishawishi serikali na wadau wa elimu kutumia bidhaa za chaki zinazotengenezwa maswa.

 

Add new comment

Plain text

  • No HTML tags allowed.
  • Lines and paragraphs break automatically.
  • Web page addresses and email addresses turn into links automatically.