Skip to main content

Rais Mpya wa Gambia Adama Barrow amteua Fatoumata Jallow Tambajang kama makamu wa rais

Rais mpya wa Gambia Adama Barrow amemteua mwanamke mwenye ushawishi mkubwa ambaye aliwahi kuwa mshirika wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Yahya Jammeh kabla ya kujiunga na upinzani ulioshinda uchaguzi kuwa makamu wake wa urais.

Aidha mwanamke huyo kwa jina Fatoumata Jallow-Tambajang amemtishia kiongozi huyo kwa kumfungulia mashtaka.

lakini watu wanatilia shaka iwapo Bi Tambajang mwenye umri wa miaka 68 anafaa kupewa wadhfa huo kutokana na umri wake.

Makamu wa Rais wa Guinea Teodorin Obiang ashtakiwa Ufaransa kwa tuhuma za kupora mali

Makamu wa rais wa Guinea Ya Ikweta Teodorin Obiang ameshitakiwa nchini Ufaransa, kwa tuhuma za kupora mali za nchi yake na kuzitumia kugharimia maisha yake ya anasa.

Obiang ambaye pia ni mtoto wa rais wa muda mrefu wa Guinea ya Ikweta, anatuhumiwa kutumia zaidi ya dola milioni 100 kutoka hazina ya serikali, kununulia jumba la kifahari katika mtaa wa matajiri mjini paris,

Mbali na jumba hilo pia amenunua magari kadhaa ya kifahari yanayotengenezwa nchini italia.

Subscribe to Africa News