Skip to main content

Wezi wavamia nyumba ya Carlos Tevez

Wezi wamevunja na kuingia katika nyumba ya aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester City Carlos Tevez viungani mwa mji wa Bueno Aires nchini Argentina siku ya jumapili na kuiba wakati nyota huyo alipokuwa nchini Uruguay kufunga ndoa.

Maafisa wa polisi wamesema kuwa Tevez hakuwasilisha ripoti kwa polisi kuhusu wizi huo hivyo haijulikani mali iliyoibwa

Tevez na mke wake tayari wameondoka na kuelekea Mexico kwa fungate yao.

Polisi wamesema kwamba wamegundua kuhusu wizi huo siku ya jumanne baada ya kuwaona wanahabari wamekusanyika nje ya nyumba ya nyota huyo.

Ligi Kuu Bara, Simba kuvaana na Ruvu Shooting.

VINARA wa Ligi Kuu Bara, Simba leo watakuwa kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam kucheza na Ruvu Shooting katika mechi inayotarajiwa kuwa ya kuvuta nikuvute.

Mechi hiyo ambayo Simba ipo ugenini, inatarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake huku mashabiki wa soka wakitamani kuona mwenendo wa Simba kama utaendelea au utaishia njiani kama ilivyo kawaida yake katika misimu iliyopita kufanya vizuri na kuvurunda mwishoni.

Ligi Kuu Bara Yanga yakaa sawa, yaipiga Ndanda 4-0.

YANGA jana ilijiongezea pointi tatu muhimu baada ya kuifunga Ndanda Fc mabao 4-0 katika mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Ushindi huo umekuja baada ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu kutoka sare ya bao 1-1 na African Lyon katika mechi iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita na hivyo kupunguzwa kasi ya kuelekea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu, nafasi inayoshikiliwa na Simba.

Azamfc yawatimua makocha wake wote, kutangaza wapya.

Uongozi wa klabu ya soka ya Azam umemtupia virago kocha wake Mhispania Zeben Hernandez baada ya timu hiyo kuwa na mwenendo mbaya kwenye Ligi Kuu.

Azam ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 27, timu hiyo haina mwenendo mzuri tangu kuanza kwa msimu huu na licha ya usajili iliofanya bado imekuwa haipati matokeo ya kuridhisha.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Azam zilizopatikana jana jioni zilisema Hernendez pamoja na wasaidizi wake wote kutoka Hispania wametupiwa virago.

Timu za soka za Simba na Yanga zazuiwa kutumia Uwanja wa Taifa

Timu za soka za Simba na Yanga za Jijini Dar es Salaam zimezuiwa kutumia Uwanja wa Taifa kwa muda usiojulikana kutoka na mashabiki wao kusababisha uharibifu wa miumbombimu ya Uwanja  wa Taifa yakiwemo mageti ya kuingilia Uwanjani na kung’oa viti kwa upande wa mashabiki wa Simba.

Uamuzi huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam  na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akikagua na kutembelea maeneo yalioathirika na uharibifu uliofanywa na mashabiki wa Simba na Yanga katika mechi iliyochezwa Octoba Mosi 2016 katika Uwanja wa Taifa.

Subscribe to Sports