Skip to main content

Ofisi ya katibu tawala Mkoa Mwanza yatakiwa kuwachukua wafanyikazi sita kutoka chuo cha Mirongo

Ofisi ya katibu tawala Mkoa wa Mwanza imetakiwa kuwachukua wafanyakazi tisa waliokuwa wakifanya kazi katika chuo cha ufundi Mirongo na kupangiwa kazi nyingine.

Mkuu wa Mkoa huo John Mongela ametoa agizo hilo baada ya kutembelea chuo hicho na kubaini wafanyakazi hao hawana majukumu ya kufanya tangu mwaka 2011 baada ya chuo hicho kufungwa.

Mkoani umeanza mkakati kukifufua chuo hicho ambacho kimetelekezwa.

Makamu wa pili wa rais Zanzibar Seilo Ali akutana na balozi mdogo wa China aliepo Zanzibar Xie Xiaolon

Makamu  wa pili wa rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi ameupongeza uongozi wa ubalozi mdogo wa jamhuri ya watu wa China uliopo Zanzibar kwa kuratibu ratiba ya ziara yake ya siku tano aliyoifanya hivi karibuni nchini China.

Amesema kuwa ziara hiyo ilimpa fursa ya kukutana na uongozi wa makampuni  na taasisi mbalimbali za China zilizoonesha nia ya kutaka kuwekeza visiwani zanzibar.

Balozi Seif Ali Iddi amesema hayo wakati wa mazungumzo yake na balozi mdogo Xie Xiaolon  ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar.

Wakala va vipimo nchini kuweka stika katika mizani zote ili kudhibiti udanganyifu

Wakala wa vipimo nchini wanatarajiwa kuweka stika katika mizani zote zilizohakikiwa na mamlaka hiyo nchi nzima ili kudhibiti udanganyifu wa wafanyabiashara wasio waaminifu wanaowaibia walaji kupitia mizani,

Kaimu Mkurugenzi huduma za ufundi wakala wa vipimo Stellah Kahwa amesema ubora wa stika hizo hauwezi kughushiwa na kuendelea kuwapa nafasi nzuri walaji.

Uwekaji wa stika hizo maalum utaanza rasmi mapema mwakani, ikiwa ni njia mojawapo ya kwenda na teknolojia ya kisasa ya kuhakikisha mteja analindwa kwa kununua bidhaa inayoendana na kiwango cha fedha aliyotoa.

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa awataka wakaazi wa Lindi kulima zao la alizeti kwa wingi

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa amewataka wakazi wa mkoa wa Lindi kulima zao la alizeti kwa wingi baada ya serikali kupata mwekezaji wa kununua zao hilo na kwa bei nzuri.

Ametoa mwito huo wakati akizungumza na wananchi wa vijiji mbalimbali vya wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi ambako amepita kuwasalimia wananchi wa jimbo lake na kuhimiza kazi za maendeleo akiwa katika siku nne za mapumziko ya mwisho wa mwaka

Wananchi wa Jimbo la Ruangwa wapewa wiki mbili kuhakikisha wanajenga vyoo kujiepusha na Kipindupindu

Wananchi wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi wamepewa wiki mbili kuhakikisha kuwa wanajenga vyoo ili kujiepusha na ugonjwa wa kipindupindu.

 

Mwito huo umetolewa na mkuu wa mkoa huo, Godfrey Zambi kwa mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Joseph Mkirikiti kuwa afanye msako wa nyumba kwa nyumba ifikapo januari 15 mwakani na awatoze faini watakaoshindwa kujenga vyoo vya kisasa

 

Watu wawili wafariki na wengine 30 kulazwa kutokana na kulipuka kwa ugonjwa wa kipindupindu Singida

Watu wawili wamefariki na wengine 30 wamelazwa kwenye vituo mbalimbali vya afya vya halmashauri ya wilaya ya Singida kwa ajili ya matibabu, tangu ugonjwa wa kipindupindu uanze kulipuka Novemba 26, mwaka huu.

Mkuu wa wilaya ya Singida Elias Tarimo amesema kuwa ugonjwa huo umebainika kulipuka katika vijiji vya Merya na Msange, tangu mwezi uliopita, lakini mamlaka zimekifanya kuwa siri

Subscribe to Tanzania New