Skip to main content

Hospitali teule ye Rubya katika wilaya ya Muleba mkoani Kagera inahitaji shilingi milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya akinamama

Hospitali teule ye Rubya katika wilaya ya Muleba mkoani Kagera inahitaji shilingi milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya akinamama wanaojifungua ili kupunguza msongamano wa katika hospitali hiyo.

Mganga mkuu wa hospitali hiyo Dokta George Kasibante amesema kuwa wajawazito wanaofujifungulia hospitalini hapo ni kati ya 300 hadi 360 kila mwezi tofauti idadi ya wajawazito 120   waliokuwa wamelengwa kuweza kuhudumiwa na hospitali

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wajumbe wa baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) wakutane na wamiliki wa taasisi za kifedha ili kuangalia uwezekano wa kutoa mikopo yenye gharama nafuu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wajumbe wa baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) wakutane na wamiliki wa taasisi za kifedha ili kuangalia uwezekano wa kutoa mikopo yenye gharama nafuu.

Ametoa kauli hiyo leo alipokutana na wajumbe wa baraza hilo katika makazi ya waziri mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam.

Waziri mkuu amesema kuwa ni vema wajumbe hao wakakutana na wamiliki wa taasisi hizo ili kuwasaidia wananchi kupata mikopo yenye masharti nafuu itakayoza uchumi wao.

Wananchi wa Tabora watakiwa kulima mazao yanayohimili ukame

Chama cha Mapinduzi ( CCM)  wilaya ya nzega mkoani tabora kimewetaka wananchi kulima mazao yanayo himili ukame ilikukabiliana na baa la njaa linaloweza kujitokeza.

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya Amos Majile ametoa kauli hiyo katika kijiji cha Mwamalulu kata ya nata baada ya kuona hali ukame imekithili.

Amesema kuwa chama cha mapinduzi hakikotayari kuona wananchi wake wanapata njaa badala yake wajihami kwa kulima mazao yanayohimili ukame ilikuweza kukabiliana na baa hilo.

Jamii yashauriwa kujiunga ya vikundi vya uwekezaji wa fedha

Jamii  imeshauriwa kujiunga na vikundi vya uwekezaji wa fedha vitanavyowawezesha wananchi kupata mikopo ya uanzishaji wa miradi ya maendeleo, itakayosaidia kupunguza hali ngumu ya maisha.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela, ametoa rai hiyo wakati akizindua kikundi cha akiba na mikopo cha “umoja vicoba”, kinachoundwa na wanahabari pamoja na wadau wa sekta ya habari.

Mkuu wa wilaya ya Chake Chake Salama Mbarouk awataka watendaji wa serikali kubadilika na kufanya kazi kwa ufanisi

Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Salama Mbarouk Khatibu amewataka watendaji wa serikali kubadilika na kufanya kazi kwa ufanisi ikiwemo kila mmoja kutekeleza majukumu yake.

Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na watendaji wa serekali mara baada ya kumaliza kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za kusherehekea miaka 53 ya mapindunzi ya zanzibar Lengo la kufanya usafi ni kuweka mazingira bora katika ofisi hivyo ni vyema wafanyakazi wakaonesha ushirikiano wao katika kutekeleza majukumu hayo.

Wafanyibiashara wa Tanzania bara na visiwani washauriwa kuwa na ushurikiano

Wafanyabiashara wa Tanzania bara na visiwani wameshauriwa kuwa na ushirikiano wa kiabiashara ikiwemo  kubadilishana ujuzi ili kuendelea kuimarisha na kudumisha muungano.

Waziri wa elimu na mafunzo ya amali Riziki Pembe ametoa rai hiyo wilaya ya Maswa mkoani Simiyu alipokuwa akiingia makubaliano na kiwanda cha kutengeneza chaki cha Maswa.

Kufuatia makubaliano hayo kupitia wizara ya elimu na mafunzo ya amali vijana wake watapata mafunzo ya namna ya kutengeneza chaki kutoka kiwandani hapo

Subscribe to Tanzania New