Skip to main content
Waziri Augustine Mahiga na balozi akipokea mswaada huo kutoka kwa balozi wa korea nchini Song Geum young.

Serikali ya Korea yatoa msaada wa zaidi ya shillingi Millioni 108 kwa wahanga wa tetemeko la ardhi Kagera

Serikali ya korea imetoa msaada wa zaidi ya shilingi milioni 108 kwa ajili ya kusaidia wahanga wa tetemeko la ardhi mkoani kagera.

 

Msaada huo umekabidhiwa kwa waziri wa mambo ya nje, ushirikiano wa Afrika mashariki, kikanda na kimataifa, Augustine Mahiga na balozi wa korea nchini Song Geum young.

 

Amesema Tanzania na Korea serikali zimekuwa zikishirikiana kwa karibu hivyo kwa kutoa msaada huo ni njia mojawapo wapo ya kudumisha uhusiano ulipona kusaidia kujenga miundombinu iliyoharibiwa na tetemeko hilo.

 

Mheshimiwa Mahiga amesema kuwa atahakikisha msaada huo unawafikia walengwa ili wakabiliane na tatizo la miundombinu iliyoharibiwa

 

Tetemeko hilo la ardhi lilitokea septemba 10, mwaka huu mkoani kagera na kusababisha vifo vya takribani watu wanane na majeruhi zaidi ya mia moja huku wengine wakipoteza makazi yao.

 

Add new comment

Plain text

  • No HTML tags allowed.
  • Lines and paragraphs break automatically.
  • Web page addresses and email addresses turn into links automatically.