Skip to main content
Makamu wa rais Mteule wa Gambia Fatoumata Jallow-Tambajang

Rais Mpya wa Gambia Adama Barrow amteua Fatoumata Jallow Tambajang kama makamu wa rais

Rais mpya wa Gambia Adama Barrow amemteua mwanamke mwenye ushawishi mkubwa ambaye aliwahi kuwa mshirika wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Yahya Jammeh kabla ya kujiunga na upinzani ulioshinda uchaguzi kuwa makamu wake wa urais.

Aidha mwanamke huyo kwa jina Fatoumata Jallow-Tambajang amemtishia kiongozi huyo kwa kumfungulia mashtaka.

lakini watu wanatilia shaka iwapo Bi Tambajang mwenye umri wa miaka 68 anafaa kupewa wadhfa huo kutokana na umri wake.

Bi. Tambajang amewahi kuhudumu kama waziri wa afya na masuala ya kijamii wakati wa utawala wa Yahya Jammeh lakini akalazimika kwenda mafichoni baada ya kukosana naye.

Baadaye alikuwa kiungo muhimu katika kuanzisha upinzani uliomshinda Jammeh mnamo tarehe mosi mwezi disemba, na alikuwa wa kwanza kumtishia kwamba atamfunguliwa mashtaka kwa uhalifu aliotekeleza wakati wa utawala wake

Add new comment

Plain text

  • No HTML tags allowed.
  • Lines and paragraphs break automatically.
  • Web page addresses and email addresses turn into links automatically.