Skip to main content
Mkuu wa wilaya ya Chake Chake Salma Mbarouk

Mkuu wa wilaya ya Chake Chake Salama Mbarouk awataka watendaji wa serikali kubadilika na kufanya kazi kwa ufanisi

Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Salama Mbarouk Khatibu amewataka watendaji wa serikali kubadilika na kufanya kazi kwa ufanisi ikiwemo kila mmoja kutekeleza majukumu yake.

Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na watendaji wa serekali mara baada ya kumaliza kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za kusherehekea miaka 53 ya mapindunzi ya zanzibar Lengo la kufanya usafi ni kuweka mazingira bora katika ofisi hivyo ni vyema wafanyakazi wakaonesha ushirikiano wao katika kutekeleza majukumu hayo.

Amewataka watendaji wa serikali kuenzi na kuthamini mapindunzi ya mwaka 1964 kwa kuendelea kudumisha amani na utulivu ndani ya nchi. Sherehe za mapindunzi zinalenga kuzindua wa miradi ya maendeleo hivyo serekali imejipanga kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi wake .

Add new comment

Plain text

  • No HTML tags allowed.
  • Lines and paragraphs break automatically.
  • Web page addresses and email addresses turn into links automatically.