Skip to main content
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dokta Kebwe Steven

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dokta Kebwe awagiza watuishi wote wa hamashauri ya wilaya kuhamia kata ya Mvuha

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dokta Kebwe Steven ameagiza watumishi wote wa halmashauri ya wilaya ya Morogoro kuhamia kata ya Mvuha kunako jengwa makao makuu ya wilaya hiyo kabla ya kufikia disemba 29 mwaka huu.

Bwana Kebwe ametoa kauli hiyo kwa niaba ya waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa [tamisemi] George simbachawene

Amesema hayo katika baraza la dharura lililo wakutanisha wakuu wa idara, madiwani pamoja na watumishi wa halmashauri hiyo mkuu wa mkoa wa morogoro

Dokta Kebwe Steven amesema waziri Simbachawene amefikia uamuzi huo baada ya agizo la awali alilo toa zaidi ya miezi sita iliyo pita kutotekelezwa.

Madiwani walio hudhuria katika baraza hlo wameunga mkono maagizo hayo wakisema kilicho kuwa kikichelewesha utekelezaji wa kuhamisha halmashauri hiyo ni kutokana na kukosekana usimamizi wa karibu toka serikali kuu.

Add new comment

Plain text

  • No HTML tags allowed.
  • Lines and paragraphs break automatically.
  • Web page addresses and email addresses turn into links automatically.