Skip to main content
Makamu wa rais wa Guinea Teodorin Obiang

Makamu wa Rais wa Guinea Teodorin Obiang ashtakiwa Ufaransa kwa tuhuma za kupora mali

Makamu wa rais wa Guinea Ya Ikweta Teodorin Obiang ameshitakiwa nchini Ufaransa, kwa tuhuma za kupora mali za nchi yake na kuzitumia kugharimia maisha yake ya anasa.

Obiang ambaye pia ni mtoto wa rais wa muda mrefu wa Guinea ya Ikweta, anatuhumiwa kutumia zaidi ya dola milioni 100 kutoka hazina ya serikali, kununulia jumba la kifahari katika mtaa wa matajiri mjini paris,

Mbali na jumba hilo pia amenunua magari kadhaa ya kifahari yanayotengenezwa nchini italia.

Teodorin Obiang, Kapela mwenye umri wa miaka 47 hakuwepo mahakamani wakati yakisomwa mashtaka dhidi yake, na wakili wake ameomba muda zaidi wa kuandaa utetezi.

Mahakama imesema itaamua kesho kuhusu ombi hilo la kuahirishwa kwa kesi, ambalo shirika la kimataifa dhidi ya rushwa, Transparency International limesema ni mbinu ya kuchelewesha haki kutendeka.

 

 

Add new comment

Plain text

  • No HTML tags allowed.
  • Lines and paragraphs break automatically.
  • Web page addresses and email addresses turn into links automatically.