Skip to main content
Balozi Mdogo wa Jamuhuri ya Watu wa China aliyepo Zanzibar Bwana Xie Yunliang alipokutana na Makamu wa rais wa pili Seif Ali Iddi

Makamu wa pili wa rais Zanzibar Seilo Ali akutana na balozi mdogo wa China aliepo Zanzibar Xie Xiaolon

Makamu  wa pili wa rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi ameupongeza uongozi wa ubalozi mdogo wa jamhuri ya watu wa China uliopo Zanzibar kwa kuratibu ratiba ya ziara yake ya siku tano aliyoifanya hivi karibuni nchini China.

Amesema kuwa ziara hiyo ilimpa fursa ya kukutana na uongozi wa makampuni  na taasisi mbalimbali za China zilizoonesha nia ya kutaka kuwekeza visiwani zanzibar.

Balozi Seif Ali Iddi amesema hayo wakati wa mazungumzo yake na balozi mdogo Xie Xiaolon  ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar.

Amesema kwamba mikutano  ya pamoja kati ya ujumbe wa Zanzibar na uongozi na makampuni mbalimbali waliyokutana nayo yalikuwa na mwelekeo mwema wa ushirikiano.

Naye balozi mdogo huyo amesema kuwa zanzibar na china daima zitaendelea kushirikiana katika miradi ya pamoja ili kuleta ustawi wa wananchi

 

Add new comment

Plain text

  • No HTML tags allowed.
  • Lines and paragraphs break automatically.
  • Web page addresses and email addresses turn into links automatically.