Skip to main content
Rock City Mall

Kanda ya ziwa watakiwa kuwekeza Rock City Shopping Mall

Wakazi wa jiji la Mwanza na kanda ya ziwa wamehimizwa kuchangamkia fursa zinazopatikana kupitia kitega uchumi cha Rock City Shopping Mall kinachotajwa kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia biashara za huduma na bidhaa.

Imeelezwa kuwa Uwekezaji zaidi unaoendelea kudhihirika katika kitega uchumi hicho ukitumiwa vyema na wakazi wa kanda ya ziwa utakuwa chachu ya mabadiliko ya kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Uwekezaji katika jengo hili umekwishatoa fursa za ajira kwa watu wapatao mia tatu hivyo kuendelea kwa uwezekezaji zaidi kunafungua milango mipana ya vichocheo vya uchumi kama vile ajira,huduma bora na kipato cha uhakika kwa watu wa kada mbalimbali.

Add new comment

Plain text

  • No HTML tags allowed.
  • Lines and paragraphs break automatically.
  • Web page addresses and email addresses turn into links automatically.