Skip to main content
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela

Jamii yashauriwa kujiunga ya vikundi vya uwekezaji wa fedha

Jamii  imeshauriwa kujiunga na vikundi vya uwekezaji wa fedha vitanavyowawezesha wananchi kupata mikopo ya uanzishaji wa miradi ya maendeleo, itakayosaidia kupunguza hali ngumu ya maisha.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela, ametoa rai hiyo wakati akizindua kikundi cha akiba na mikopo cha “umoja vicoba”, kinachoundwa na wanahabari pamoja na wadau wa sekta ya habari.

suala la uwekezaji wa fedha katika karne hii kamwe halikwepeki, na kuwa jambo muhimu ni uwepo wa wanachama waaminifu na wenye nidhamu ya fedha, watakaowezesha kundi kufikia malengo ya mpango husika wa uwekezaji.

mwenyekiti wa “umoja vicoba” Frenk Leonard amesema kikundi hicho mwaka 2015 kilianza kwa wanachama kuwekeza kiasi cha shilingi milioni 40, na sasa “umoja vicoba” imefanikiwa   kuwekeza zaidi ya shilingi milioni 75.

Aidha Leonard amesema awali lengo la kikundi lilikuwa ni kuweka akiba ya shilingi milioni 100 ikiwa pamoja na kuanzisha miradi ya maendeleo, na jambo hilo limekwama kutokana na hali ngumu ya kiuchumi

Add new comment

Plain text

  • No HTML tags allowed.
  • Lines and paragraphs break automatically.
  • Web page addresses and email addresses turn into links automatically.