Skip to main content
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotmbelea siptali ya Kagera awali

Hospitali teule ye Rubya katika wilaya ya Muleba mkoani Kagera inahitaji shilingi milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya akinamama

Hospitali teule ye Rubya katika wilaya ya Muleba mkoani Kagera inahitaji shilingi milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya akinamama wanaojifungua ili kupunguza msongamano wa katika hospitali hiyo.

Mganga mkuu wa hospitali hiyo Dokta George Kasibante amesema kuwa wajawazito wanaofujifungulia hospitalini hapo ni kati ya 300 hadi 360 kila mwezi tofauti idadi ya wajawazito 120   waliokuwa wamelengwa kuweza kuhudumiwa na hospitali

Amesema hayo katika kupokea tuzo ya utoaji bora wa huduma ya mama na mtoto iliyotolewa leo na shirika la JHIPIEGO  mkoani humo na kwamba kipindi cha miezi sita kati ya june hadi desemba 2016 wamejifungua wanawake 2,057.

Afisa mipango wa shirika la JHIPIEGO Bi Alphonciana Barongo amesema licha ya changamoto za hospitali hiyo shirika bado linaipatia tuzo na cheti kwa ajili ya utoaji huduma za afya na kupunguza vifo vya mama na watoto.

 

 

 

Add new comment

Plain text

  • No HTML tags allowed.
  • Lines and paragraphs break automatically.
  • Web page addresses and email addresses turn into links automatically.