Radio Free Africa Tanzania

Hazina ya serikali, Waziri wa Fedha akanusha kufilisika.
Na James Range,

Dar es salaam.

Waziri wa fedha na Uchimi Dokta William Mgimwa amekanusha taarifa ya Waziri kivuli wa Fedha Mheshimiwa Zitto Kabwe kuwa Hazina ya Serikali imefilisika na kusema kuwa hazina ipo katika hali nzuri kwani ina fedha za kutosha.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Mheshimiwa Kabwe ambaye ni naibu kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema kuwa hazina ya Serikali imefilisika.

Dokta Mgimwa amefafanua kuwa hazina ya fedha za kigeni kwenye benki kuu yaTanzaniani imara na kwamba mpaka mwezi Machi mwaka huu kulikuwa na zaidi ya Dola za Kimarekani Bilioni 3.6 kwenye hazina hiyo.

Waziri Mgimwa ameongeza kuwa kiasi hicho cha akiba ya fedha za kigeni ni kigezo kinachoonesha kuwaTanzaniakamanchi ipo imara kwenye hazina yake ya fedha.

Katika waraka wake kuhusiana na kukauka kwa hazina ya taifa Mheshimiwa Kabwe alisema Benki kuu yaTanzaniailikuwa imefilisika na kwamba hela iliyopo isingetosha kuendesha nchi katika kipindi cha miezi mitatu ijayo.

Hata hivyo waraka huo wa Zitto ulipingwa vikali na Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM mwigulu Nchemba kwa kumtuhumu mbunge huyo kuwa anapotosha Taifa.

Mwisho.

Tweet This Post

NHC kupandisha kodi kwa asilimia 35.
Na Emmanuel Michael,

Singida.

Shirika la Nyumba la Taifa NHC linakusudia kupandisha kodi ya nyumba kwa wapangaji wake hadi kufikia asilimia themanini na tano ya bei ya soko ifikapo mwaka 2015.

Lengo la hatua  hiyo  ni kuhakikisha kuwa shirika  hilo linaongeza zaidi mapato  yake kwa ajili ya kujenga nyumba nyingine  za kupangisha  pamoja na kuwauzia Watanzania wengi.

Mkurugenzi mkuu wa shirikahiloBwana Nehemiah Mchechu amekiambia kikao cha Baraza kuu la Wafanyakazi mjini Singida kuwa, mpango huo wa kupandisha kodi unakusudia kuongeza mapato.

Amesema hatua  hiyo ni moja ya njia za kupata fedha kwa ajili ya kutekeleza mkakati wa shirika  hilo katika  kujenga nyumba elfu kumi na tano  kote nchini ifikapo mwaka 2015.

Akifunga kikao hicho cha baraza la wafanyakazi wa shirika la nyumba la taifa, Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Kone ametaka kutekelezwa ipasavyo kwa mikakati iliyowekwa.

Zaidi ya wajumbe 70 kutoka maeneo mbalimbali nchini wamehudhuria kikao hicho cha baraza kuu la wafanyakazi  wa shirika la nyumba la taifa kilifanyika mjini Singida kwa siku mbili.

Mwisho

Tweet This Post

Mahakama ya Kisutu yahairisha kutoa hukumu kesi ya Maranda.
Na Immaculate Kilulya,

Dar es Salaam.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijiniDar Es Salaamimeahirisha kutoa hukumu ya kesi ya wafanyabiashara wawili Farijala Hussein na Rajabu Maranda wanaokabiliwa na mashtaka ya kula njama, kughushi na wizi wa shilingi bilioni 2.2maliya Benki kuu ya Tanzania BOT kutoka akaunti ya madeni ya nje EPA.

Hukumu ya Kesi hiyo iliyokuwa itolewe leo imeahirishwa na hakimu wa mahakama hiyo Catherine Revocatus kutokana na mahakimu wawili wanaosikiliza kesi hiyo kuwa na matatizo ya kiafya na hivyo imepangwa kufanyika Juni 26 mwaka huu.

Mahakimu wengine wanaosikiliza kesi hiyo ni Fatuma Masengi na Benedict Mwingwa ambao hawakufika mahakamani hapo na hivyo kufanya jopohilokushindwa kutimia kwa ajili ya kutoa hukumu kwa watuhumiwa hao.

Katika kesi ya msingi watuhumiwa hao wanadaiwa kujipatia shilingi bilioni 2.2 kutoka katika akaunti ya EPA kupitia kampuniyaoya Money Planners and Consultants kwa madai kuwa wamepewa kibali na kampuni B, Grancel ya nchi Ujerumani kukusanya madeni yake.

Mbali na kesi hiyo wafanyabiashara hao pia wanatumikia kifungo cha miaka mitano jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kuiibia Benki Kuu ya Tanzania B.O.T Shilingi bilioni 1.8 kupitia Akaunti ya Madeni ya nje EPA.

Watuhumiwa hao wanawakilishwa na mawakili wawili ambao ni Majura Magafu na Mabere Marando huku upande wa serikali ukiwakilishwa na Arafa Msafiri.

Mwisho.

Tweet This Post

Uvunaji mbao, Mapungufu yaikabili Sekta ya Misitu.
Na Grace Semfuko,

Dodoma.

Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda amesema bado kuna mapungufu makubwa kwenye sekta ya misitu nchini kupitia uvunaji wa mbao hatua inayodhoofisha usimamizi wa sekta ya nyuki na kulisababishia taifa hasara.

Hasara hiyo inatokana na kukosekana na fedha za kigeni kwani sekta hiyo inatumia nguvu na fedha kidogo katika uendeshaji wake.

Waziri Pinda ameyasema hayo mjini Dodoma mara baada ya kupokea ujumbe wa wafugaji kutoka mkoa wa Kusini Pemba waliofika mjini humo kwa lengo la kujifunza namna ya ufugaji bora wa nyuki.

Amesema kumekuwa na hujuma za makusudi za kuua sekta hiyo na kuitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuelekeza nguvu zao zaidi katika ufugaji wa nyuki kutokana na kuwepo rasilimali nyingi za ufugaji huo ikiwepo misitu na nyuki wa kutosha.

Kutokana na sekta ya ufugaji wa nyuki kusahaulika na mamlaka zinazohusika, Mfuko wa maendeleo ya jamii Tanzania TASAF umefadhili miradi 235 yenye thamani ya shilingi bilioni 2.5 kwax mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa TASAF nchini Ladislaus Mwamanga.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Bwana Juma Tindwa amesema lengo la ziara hiyo ni kujifunza juu ya ufugaji wa nyuki.

Mwisho.

Tweet This Post

Mabaraza ya Madiwani yahimizwa kudai taarifa za mapato.
Na Kakuru Msimu, Korogwe.

Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI imeyaagiza mabaraza ya madiwani kwenye halmashauri za miji, wilaya na majiji nchini kudai taarifa ya Mkaguzi wa Ndani ili kubaini ubadhirifu wa fedha za umma unaofanywa na baadhi ya watendaji.

Hatua hiyo itasaidia kupunguza mianya ya ufujaji wa fedha za umma kwenye miradi ya maendeleo endapo madiwani hao watatambua wajibu wao na kuwajibika ipasavyo katika kuwatumikia wananchi.

Naibu Waziri wa TAMISEMI Bw. Agrey Mwanri ametoa kauli hiyo wilayani Korogwe wakati akihitimisha mafunzo ya Madiwani kitaifa na kubainisha kuwa hakuna mtumishi atakayehamishwa ikiwa anatuhumiwa kuhusika na ubadhilifu wa fedha umma.

Mapema Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Korogwe Bwana Sadick Kallage katika taarifa yake pamoja na mambo mengine ameiomba Serikali kuboresha maslahiyaosanjari na kuanzisha mfuko wa katakamaulivyo mfuko wa Jimbo kwa waheshimiwa Wabunge.

Baadhi ya madiwani wameelezea kuwa semina hiyo imewafumbua macho na kuahidi kufanya kazi kwa uadilifu ili kuepuka hati chafu.

Mafunzo hayo yameandaliwa na TAMISEMI na kuratibiwa na sekretarieti ya Mkoa wa Tanga ambao umetoa wakufunzi waliotoa mada mbalimbali.

Mwisho.

Tweet This Post

Migogoro ya mikopo vyuoni, Serikali yatupiwa lawama.
Na Joyce Mwakalinga,

Dar Es Salaam.

Ukosefu wa mikopo kwa baadhi ya wanafunzi wa elimu ya juu nchini ambao unaleta migogoro unasababishwa na Serikali kwa kushindwa kufuatilia mikopo iliyotolewa kwa wanafunzi waliotangulia.

Kauli hiyo inakuja baada ya wanafunzi wa elimu ya juu katika baadhi ya vyuo kutawanywa na Polisi kwa mabomu ya machozi walipokuwa wakifuatilia mikopo katika Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu HELSB.

Mwenyekiti mstaafu wa umoja wa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini TAHLISO  Bwana Mathias Kipala amesema hayo alipofanya mahojiano na Star Tv jijiniDar Es Salaam.

Sanjari na kufuatilia mikopo hiyo, Bwana Kipala ameitaka Serikali kufuatilia wanafunzi wasio na uwezo na kuwapatia kipaumbele katika utoaji wa mikopo hiyo.

Fadhili Unyayo ni Afisa udahili kutoka shule ya kibiashara yaLondonnchiniTanzaniayeye anawashauri wanafunzi kupendelea kusoma vyuo vya hapa nchini na kuchagua fani zitakazowaingiza katika ajira pindi wanapomaliza masomoyao.

Kuhusiana na baadhi ya wanafunzi wanaolowea nje ya nchi mara baada ya kumaliza masomoyaoDismas Lyassa ambaye ni Afisa mtendaji wa taasisi inayowasomesha wanafunzi nje ya nchi anasema hali hiyo inatokana na maslahi ambayo hata hivyo baadaye huwa na faida kwa wananchi waTanzania.

Katika kukabiliana na matatizo mbalimbali ya vyuo vya elimu ya juu nchini taasisi ya hiyo ya Global Source Watch imeandaa maonyesho ya wanafunzi wa elimu ya juu nchini yatakayofanyika Mei 26 na 27 jijiniDar Es salaam.

Mwisho.

Tweet This Post

Waislamu Geita waukataa uongozi wa BAKWATA.
Na Wilson Elisha,

Geita.

Waumini wa dini ya Kiislamu wilayani Geita mkoani Geita wameukataa uongozi wa Baraza la Waislamu Tanzania BAKWATA ulioko madarakani kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo ubadhilifu wamaliza waumini.

Hatua hiyo imechukuliwa kwa madai kuwa viongozi hao wameshindwa kusoma mapato na matumizi kwa waumini kwa muda mrefu jambo ambalo linsababisha wasiwe waaminifu na waadilifu mbele ya waumini hao.

Wakizungumza katika kikao kilichofanyika kwenye Msikiti wa Ijumaa wilayani Geita mbele ya viongozi wa Baraza la Waislamu BAKWATA Mkoa wa Mwanza akiwemo Sheikh wa Mkoa Salum Feleji waumini hao wamesema hawana imani na viongozi hao.

Wamebainisha kuwa hata fedha zilizochangwa katika harambee iliyosimamiwa na Sheikh Mkuu waTanzaniaMufti Shabani bin Simba hazijulikani zilifanya kazi gani.

Mbali na ubadhilifu huo, viongozi hao wanatuhumiwa kwa kushindwa kuuendeleza uislam katika Wilaya ya Geita na Mkoa kwa ujumla kwani hata MADRASA hazifanyi kazi.

Kutokana na hali hiyo waumini hao wamemuomba Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shabani Bin Simba kuunda kamati mahususi ambayo itasaidia kuondoa mgogoro baina ya waumini na viongozi hao.

Akizungumzia tuhuma za kufuja fedha, Sheikh wa Wilaya ya Geita Haddi Yusufu amekanusha kuhusishwa kwa madai kuwa hazitambui na kama kuna muumini yoyote anayefahamu sualahiloatoe ushahidi.

Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Salum Feleji amesema wamekamilisha agizo la Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaban Bin Simba la kuwataka kufika wilayani Geita kusikiliza malalamiko ya waumini dhidi ya watuhumiwa.

Viongozi wanaotakiwa kuondolewa madarakani kutokana na tuhuma hizo ni Sheikh wa Wilaya Haddi Yusufu pamoja na Mwenyekiti na Katibu wa BAKWATA mkoa Said Mahuma na Said Karidushi.

Mwisho.

Tweet This Post

Zaidi ya abiria 60 wanusurika kifo Singida.
Na Emmanuel Michael,

Singida.

Zaidi ya abiria 60 wamenusurika kifo baada ya magari waliyokuwa wakisafiria kugongana katika eneo la kona ya kuingia kituo kikuu cha mabasi mjini Singida.

Ajali hiyo imetokea jana majira ya saa saba na robo mchana na kulihusisha basi la Mohamed Trans lenye namba za usajili T. 848 BEQ aina ya Scania na Toyota Hiace yenye namba za T.499 BRS.

Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Singida Kamishina msaidizi mwandamizi Celina Kaluba amesema  chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi la Mohamed Trans lililokuwa likitokea Morogoro kuelekea jijini  Mwanza kushindwa kuzingatia  taratibu na sheria za usalama barabarani.

Amesema dereva huyo ambaye hakuweza kutambulika jina wala makazi yake mara moja, ametoroka kwenda kusikojulikana baada ya ajali kutokea na polisi wanaendelea kumtafuta.

Licha ya majeruhi wengine  kutibiwa na kuruhusiwa kuendelea na safari zao, abiria wanne akiwemo dereva wa Hiace  hiyo iliyokuwa inatoka  Singida mjini  kuelekea Iglanson Singida  Vijijini  Yesaya Samson wamelazwa kutokana na kuvunjika mikono na miguu.

Mwisho

Tweet This Post

Wakazi Arusha hatarini kupata magonjwa ya mlipuko.
Enos Masanja,

Moshi.

Wananchi wa kata ya Arusha chini wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro wako hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na kuzingirwa na maji yanayotokana na mafuriko yaliyokumba maeneo ya tambarare ya wilaya hiyo.

Star Tv imezuru eneo hilo na kukutana na baadhi ya wananchi ambao walidai wako kwenye kisiwa cha nchi kavu kwa muda wa wiki moja sasa.

Pamoja na hali ya hofu ya magonjwa ya mlipuko, wananchi hao wamekuwa wakipita taabu kutoka sehemu moja kwenda nyingine kutokana na kuzingirwa na maji.

Mbunge wa viti maalumu kupitia tiketi ya CHADEMA mkoani Kilimanjaro Mheshimiwa Grace Kiwelu ameungana na Diwani wa kata ya Arusha Chini Mheshimiwa Rojas Mmari kuwapatia msaada wa gunia tano ya mahindi wahanga wa mafuriko.

Tangu zianze kunyesha kwa karibu ya mwezi mmoja sasa mvua za masika zimesababisha mafuriko katika maeneo mengi ya tambarare ya wilaya ya Moshi na huenda zikasababisha maeneo hayo pia kukumbwa na uhaba wa chakula kutokana na mazao mengi kufunikwa na maji.

Mwisho

Tweet This Post

Wakuu wa Wilaya wahimizwa kufanya usimamizi.
Na Maliganya Charahani, Mwanza

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo amewataka Wakuu wa Wilaya kusimamia kikamilifu matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo katika utendaji wa Halmashauri za Wilaya zao ili kuongeza tija na kuwanufaisha wananchi.

Akizungumza baada ya kuwaapisha Wakuu wa Wilaya saba walioteuliwa hivi karibuni, Mhandisi Ndikilo amesema Wilaya za Sengerema na Misungwi zimebainika kutumia fedha za umma vibaya katika mwaka wa fedha uliopita na hivyo kupata hati chafu kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa fedha za Serikali CAG.

Amesema watumishi wa umma wanapaswa kumwogopa Mungu ili waweze kutekeleza majukumuyaoipasavyo.

Aidha amewataka wakuu wa Wilaya kutatua migogoro ya ardhi inayozikabili wilaya hizo kwa kutoa haki sawa kwa wananchi kulingana na mgawanyo wa ardhi na sheria yake ya mwaka 1999.

Baadhi ya wakuu wa wilaya walioapishwa wameahidi kutimiza wajibu wao kwa kusimamia maslahi ya umma ili kuharakisha maendeleoyao.

Katika ukaguzi wa hesabu za serikali za mitaa uliopita, wilaya ya Sengerema imeonekana kuwa na matumizi mabaya ya fedha zaidi ya shilingi bilioni mbili na Misungwi ikifuja zaidi ya shilingi bilioni moja.

Kutokana na ufujaji huo, watendaji wake wakuu wameamriwa kufikishwa mahakamani kujibu shutuma za upotevu wa fedha hizo.

Mwisho

Tweet This Post