The Sound Of Africa
Saturday May 19th 2012

Interesting Sites

Insider

Archives

Uchaguzi Arumeru Mashariki, Daftari la Wapigakura lafanyiwa marekebisho.

Na Immaculate Kilulya,

Dar es Salaam. 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imelifanyia marekebisho madogo Daftari la Kudumu la WapigaKurakwa ajili ya uchaguzi mdogo wa ubunge kwenye jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha.

Katika marekebisho hayo, NEC imewaingiza wapiga kura 26 kwenye daftarihilona kufanya idadiyaokufikia 127, 455 kutoka 127,429 wa mwaka 2010

Taarifa za marekebisho hayo zimetolewa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Damian Lubuva ambaye amesema yamefanyika baada ya kubaini kuwepo kwa wapiga kura 54 waliojiandikisha zaidi ya mara moja na wengine vitambulisho vyao kuharibika, wakati 28 wamejitokeza zaidi ya mara moja kwenye daftarihilolililotumika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Hata hivyo Jaji Lubuva amewatoa hofu wananchi kuwa marekebisho hayo ni halali na hakuna utata wowotekamainavyodaiwa na baadhi ya wanasiasa.

Kutokana na marekebisho hayo, jumla ya watu 127, 455 wanatarajiwa kupiga kura kwenye uchaguzi huo Aprili Mosi mwaka huu katika vituo 427 vilivyopo ndani ya kata 17 za Arumeru Mashariki.

Katika hatua nyingine Jaji Lubuva amesisitiza kuwa Mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM kwenye uchaguzi huo Sioi Sumari ni mgombea halali kwa sababu ni raia waTanzania.

Amesema licha ya Sumari kuzaliwa nchiniKenyana wazazi wake kuwa Watanzania lakini hakuwa na uraia waKenyana hivyo ni mgombea halali.

Awali Machi 9 mwaka huu Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kilimwekea pingamizi mgombea huyo kwa madai kuwa siyo raia wa Tanzania bali ni raia wa nchini Kenya kabla ya tume ya taifa ya uchaguzi kulitolea ufafanuzi jambo hilo.

 

Mwisho

Related posts:

Related Ways to Take Action:
Powered by Social Actions

Leave a Reply