The Sound Of Africa
Saturday May 19th 2012

Interesting Sites

Insider

Archives

Wanachama 1,122 wa CUF Ilemela wajiondoa

Na Mwandishi wetu

Wanachama 1,122 wa Chama cha Wananchi CUF wilayani Ilemela mkoani Mwanza wamejivua Uanachama kwa madai kuwa chama hicho kina ombwe la uongozi ambao haujali maslahi ya Tanzania Bara.

Wanachama hao walioongozwa na Kaimu Mwenyekiti Wilaya, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazee Wilaya na Katibu wa Vijana wa Wilaya hiyo wamesema hawaoni umuhimu wa kuendelea kuitwa wanachama katika chama ambacho hakizingatii demokrasia na maslahi ya wengi.

Siyo kawaida kwa ofisi za vyama vya siasa kuwa zimefungwa wakati wa masaa ya kazi kwa kuwa wakati wowote zinapaswa kutoa huduma kwa wanachama wake.

Kwa CUF Wilaya ya Ilemela jambo hili limewezekana kwa kuwa hakuna tena kiongozi wa kuwasikiliza wanachama.

Madai ya kutokutolewa kwa ruzuku ya shilingi laki tatu kila mwezi ili kuendesha ofisi zilizoko wilaya 116TanzaniaBara kama ilivyoamriwa tangu Oktoba mwaka jana pamoja na kufukuzana uanachama ni miongoni mwa mambo yaliyowakera wanachama hawa hatimaye wakafikia uamuzi wa kujiengua.

Kwa mujibu wa Kaimu Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Ilemela Bwana Shaaban Itutu hawaoni sababu za kufukuzwa uanachama kwa Hamad Rashid Mohamed Mbunge wa wawi na wenzake kwa kuwa madaiyaoyalikuwa ni ya kuimarisha chama hicho.

Viongozi hawa pia wanaona chama chao kimevunja sheria namba 5 ya mwaka 1992 iliyoanzisha vyama vingi vya siasa ambavyo lengolakeni kuruhusu uhuru wa mawazo ambapo pia wanahofu juu ya serikali ya umoja wa kitaifa kuwa imedhoofisha chama chao.

Januari 3 mwaka huu viongoi hawa walitoa pendekezo kwa Baraza la chama hicho kutumia busara katika kuamua mustakabali wa Hamad Rashid Mohamed na wenzake ombi ambalo wanaliona kuwa lilipuuuzwa na hatimaye maamuzi ya kuwafukuza uanachama yakachukuliwa Januari 4.

           

Mwisho

Related posts:

Related Ways to Take Action:
Powered by Social Actions

Leave a Reply