The Sound Of Africa
Thursday February 23rd 2012

Interesting Sites

Insider

Archives

Kuingizwa hifadhi ya Saadani, Wananchi Pangani wailalamika Serikali

Na Omar Masoud,                                          

Dar es Salaam. 

Wananchi wa kijiji cha Mbulizaga katika kata ya Mkaramo wilayani Pangani mkoani Tanga wameilalamikia Serikali kwa madai ya kuingiza maeneoyaokwenye Hifadhi ya Saadani hatua inayowarudisha nyuma kimaendeleo.

Wananchi hao ambao wanaishi kando ya hifadhi hiyo wanadai uporaji huo wa ardhi umekuwa ukifanyika kwa muda mrefu huku malalamikoyaoyakiendelea kupuuzwa na baadhi ya viongozi wa Serikali.

Malalamiko haya ya wananchi wa kijiji cha Mbulizaga yanatolewa mbele ya Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Ezekiel Maige aliyefika kijijini hapo kukagua utunzaji wa vivutio mbalimbali vya utalii mkoani Tanga.

Kilio cha wananchi hao walichokitoa kwa lengo la kumfahamisha Waziri Maige tatizo linalowakabili ili kulipatia ufumbuzi kilikuwa ni mwendelezo wa kauli za aina hiyo zilizotolewa hapo kabla na Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bibi Zepoza Pangani na Mbunge wa Pangani Mheshimiwa Salehe Pamba wakati Waziri huyo alipokuwa akipewa taarifa kuhusu hali ya vivutio vya kitalii wilayani humo.

Maneno hayo yanayoshabihiana baina ya Wananchi na Viongozi hao yanamshtua Waziri Maige ambaye sasa anafunguka macho na kung’amua kuwa huenda taarifa aliyopewa hapo awali na Mamlaka zinazohusika na masuala ya Hifadhi hiyo kuwa hakuna tatizo lolote katika eneohilosiyo sahihi.

Kwa kauli hii, wananchi hawa wa kijiji cha Mbulizaga sasa wanapata matumani kuwa huenda kero hiyo itapatiwa ufumbuzi huku wakihimiza uadilifu na kujali maslahi ya umma katika kulipatia ufumbuzi sualahilo.

Katika ziara hiyo Waziri Maige amefanikiwa kukagua utunzaji wa vivutio mbalimbali mkoani Tanga ikiwemo Misitu hasa miti ya mikoko, Mbuga ya Saadan, fukwe ya bahari ya Hindi, mapango na maeneo mengine muhimu.

 

Mwisho

Related posts:

Related Ways to Take Action:
Powered by Social Actions

Leave a Reply