Na Mwandishi Maalum, Arusha.
Vyama vya siasa 158 kutoka nchi wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki vinatarajiwa kuhudhuria mkutano wa kwanza jijini Nairobi Kenya kuanzia septemba 15 mwaka huu.
Naibu Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo anayeshughulikia shirikisho la kisiasa, Beatrice Kiraso amesema vyama hivyo vina jukumu la kuhamasisha ushirikiano wa kiuchumi na kisiasa.
Amesema mkutano huo utatoa nafasi kwa vyama husika kuchunguza ilani zao na kupendekeza njia zitakazowezesha kushiriki katika siasa za kanda ya Afrika Mashariki.
Mambo mengine yatakayojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na usajili, demokrasia ndani ya vyama vya siasa, na jinsi ya kukuza amani na utulivu katika jumuiya hiyo.
Mwisho.










