Na Jovita Kaijage, Dodoma.
Shirika la Hakielimu la jijini Dar-es- salaam limetoa nakala elfu ishirini za katiba zenye thamani ya shilingi milioni 19 kwa wananchi na taasisi mbali mbali nchini.
Nakala hizo zimetolewa katika kipindi cha kuanzia mwezi mei mwaka huu hadi sasa.
Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Mkurugenzi wa shirika hilo Bi. Elizabelt Missokia wakati akizungumza katika mkutano mkuu wa mwaka wa marafiki wa elimu kutoka mikoa ya tanzania bara mjini Dodoma.
Amesema mbali na shirika hilo kuendelea kuwajengea uwezo wanaharakati wa masuala mbali mbali hapa nchini wanatambua kuwa moja ya nyenzo muhimu wanazotakiwa kuwa nazo ni katiba.
Amefafanua kuwa idadi kubwa ya wananchi wanashindwa kutimiza wajibu wao kwakuwa hawatambui haki na wajibu wao.
Shirika la Hakielimu lililoanzishwa mwaka 2001 likiwa na watu 13 hivi sasa lina marafiki wa elimu 35,353 nchini kote.
Mwisho










