The Sound Of Africa
Saturday May 19th 2012

Interesting Sites

Insider

Archives

Serikali kutekeleza miradi ya maji mkoani Dodoma.

Na Seda Elias na Deborah Mpagama, Dodoma

Serikali kwa kushirikiana na benki ya dunia na jamii ipo katika mchakato wa utekelezaji wa miradi ya maji katika vijiji vya Dodoma.

Naibu Waziri wa Tamisemi  Mheshimiwa Agrey Mwary amesema hay0 wakati akijibu swali la Mbunge  David Mchiwa Malole.

Amesema utafiti wa maji na  ardhi umeshafanyika pamoja na uchimbaji wa visima na vipimo vya wingi wa maji.

Amefafanua kuwa fedha za miradi  hiyo  zilitengwa katika bajeti ya mwaka 2010 – 2011.

Aidha  katika mwaka wa fedha wa 2011 – 2012 serikali kupitia halmashauri  ya manispaa ya Dodoma imeweka kipaumbele katika kuboresha kilimo cha mbogamboga katika Halmashauri hiyo kwa kujenga kuta za kinga maji kwenye mito ya msimu.

Wakati huo huo serikali  imesema kuwa kwa sasa haitajenga  barabara kutoka Namanyere hadi Karando mkoani Rukwa kwa kiwango cha lami

Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa John Magufuli  amesema hayo wakati akijibu swali bungeni leo mjini Dodoma.

Amesema kuwa katika mkoa wa Rukwa kwa sasa kuna barabara nyingi ambazo zinatengenezwa kwa kiwango cha lami.

 

Mwisho.

Related posts:

Related Ways to Take Action:
Powered by Social Actions

Leave a Reply