The Sound Of Africa
Saturday May 19th 2012

Interesting Sites

Insider

Archives

Mwanri aagiza DED Bunda kumchukuli​a hatua mhandisi wa ujenzi.

Na Ahmed Makongo, Mugumu-Serengeti. 

 
SERIKALI imemtaka mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Bunda, mkoani Mara, kumchukulia mara moja hatua za kinidhamu, mhandisi wa ujenzi wa wilaya hiyo, Mwita Mhechi, kwani amekuwa atekelezi wajibu wake ipasavyo na kusababisha baadhi ya miradi kutokuwa na kiwango kinachotakiwa.
 
Agizo hilo lilitolewa na Naibu Waziri ofisi ya Waziri mkuu Tawala za mikoa na serikali za Mitaa (Tamisemi), Agrrey Mwanri, kwenye kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani Mara, kilichofanyika mjini Mugumu, wilayani Serengeti.
 
Naibu Waziri Mwanri, amesema kuwa katika ziara yake aliyoifanya katika wilaya ya Bunda, aligundua kuwa mhandisi wa ujenzi katika wilaya hiyo, atekelezi wajibu wake ipasavyo, kwani baadhi ya majengo katika halmashauri hiyo hayana ubora unaotakiwa, ambapo utekelezaji wake ulifanyika chini ya usimamizi wa mahandisi huyo.
 
Kufuatia hali hiyo, Naibu Waziri huyo alimwagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Cyprian Oyier, kuhakikisha anamchukulia hatua za kinidhamu mhandisi huyo, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha anampelekea vyeti vyote vya elimu yake (CV) vya mhandisi huyo ndani ya kipindi cha miezi mitatu, ili aweze kujiridhisha kama anazo sifa zinazostaili kuwa mhandisi.
 
Amesema kuwa jengo moja la ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo ambalo limegharimu mamilioni ya fedha, milango yake aina ubora kwani mbao zilizotumika si za mwininga kama mkataba ulivyokuwa unasema na badala yake zimewekwa mbao nyingine na kupigwa rangi ili zionekane kuwa ni imara, jambo ambalo alisema hiyo ni njia ya kuiba fedha za halmashauri hiyo.
 
Ameongeza kuwa wakati anakagua jengo hilo aligundua mapungufu mengi, ikiwa ni pamoja na vitasa kutokuwa na uimara unaotakiwa na kwamba awali mahandisi huyo alimdanganya kwamba vinauimara, lakini baada yakumbana alikubali kuwa si imara.
 
Aidha, Mwanri amesema kuwa hilo ni agizo ni kwa wahandisi wote nchini ili kuhakikisha kwamba wanatekeleza wajibu wao ipasavyo wa kusimamia majukumu waliyopewa.

 
Naibu waziri pia ametoa maagizo mbalimbali, likiwemo la kutokutoza ushuru kwa wafanyabiashara ndogondogo, kwani vyanzo hivyo vilikwishafutwa na serikali.
 
Amesema ushuru huo uko kwenye vyanzo vilivyofutwa na serikali na kwamba fedha hizo zimekuwa zikililetwa na serikali kuu kufidia vyanzo hivyo na kuonya kuwa iwapo akigundua kuwa bado kuna halmashauri inatoza ushuru huo, mkurugenzi wake atachukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kutoletewa fedha hizo.
 
Pia Mwanri ameziagiza halmashauri zote mkoani Mara, hususani halmashauri ya wilaya ya Serengeti, kuongeza mapato ya ndani ambapo pia amekemea tabia ya fedha za miradi ya maendeleo kukaa benki bila kutekeleza mradi uliokusudiwa.
 
Wakati huo huo, akijibu hoja ya jengo la mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bunda, kwamba limezidiwa na jengo la ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Bunda, ambalo limetumia fedha kidogo, mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo, Bw. Joseph Malimbe, amesema jingo hilo limegharimu fedha nyingi kiasi hicho kwa sababu ni kubwa kuliko ofisi ya mkuu wa wilaya.
 
Mwisho

Related posts:

Related Ways to Take Action:
Powered by Social Actions

Reader Feedback

One Response to “Mwanri aagiza DED Bunda kumchukuli​a hatua mhandisi wa ujenzi.”

  1. TANU MASHAURI says:

    hoja ya waziri kwamba mhandis onyeshe vyeti vyake sio ya msingi kwasabab vyeti ni just written material na sio kigezo cha kudhihilisha uwezo wa mtu inawezekana huyo mhandis alikalili tu then akafaulu mtihan so cha msingi ni kupima compitance ya mtu kwa vitendo, na swala jingine inawezekana kuwa huyo mhandis hukutumia proportional inayotakiwa kwa makusudi na hivyo kujinufaisha yeye mwenyewe mali ya uma.

Leave a Reply