The Sound Of Africa
Saturday May 19th 2012

Interesting Sites

Insider

Archives

Mgogoro wa kidini waibuka Kisarawe.

Na Julieth Ngarabali,Kisarawe.
 
UONGOZI wa wilaya ya Kisarawe Mkoani  Pwani umelazimika kumuhamisha kituo cha kazi mwalimu mkuu wa shule ya msingi jina tunalo(Sungwi)baada ya kutuhumiwa kuwa ni chanzo cha kuzuka kwa mgogoro ya kidini wilayani humo.
 
Mwalimu huyo jina tunalo anadaiwa kusababisha kuzuka mgogoro mkubwa wa kidini ya kiislamu na kikristo kwenye kijiji cha Sungwi na kisha baadae kusambaa hadi vijiji vingine vitatu wilayani humo
 
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari mgogo huo wa kidini ulienea kwanza kwenye kijiji cha Sungwi na baadae ukaingia pia katika vijiji vya Masaka,Kisanga na Kisarawe yenyewe.
 
Imedaiwa kuwa chanzo cha mgogoro huo ni pale mwalimu huyo alipokorofishana na mwanafunzi wa  kike anayeabudu uislamu anayesoma darasa la saba shuleni hapo na katika majibizano ndipo wawili hao walipopishana kauli.
 
Imeelezwa mwanafunzi huyo aliporudi nyumbani kwao alipeleka malalamiko kwa wazazi wake kuwa  katika majibizano yaliyotokea shuleni, mwalimu huyo alitumia lugha na maneno ya kashfa ambayo  inaidhalilisha dini ya Uislamu. 
 
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Absalom Mwakyoma alipoulizwa kuwepo tukio hilo amethibitisha mwalimu huyo kuhamishhwa kituo cha kazi kwa maelezo yanayofanana na ya chanzo chetu hicho cha habari.
 
Amesema fukuto la kuchukiwa mwalimu huyo kwa madai hayo lilianza mwishoni mwa mwezi  Februari na ikawa inakua polepole hadi majuzi ilipobainika kuwepo na watu katika vijijini vingine  vitatu ambao wanadaiwa wana hasira na mwalimu huyo huku kukiwepo tayari na tukio la kutaka kumteketeza kwa moto.
 
Akielezea tukio hilo Mwakyoma amesema wiki iliyopita watu wasiofahamika majina wala idadi walivamia nyumbani kwa mwalimu huyo na  kupanga viti na nyasi nyingi kwenye mlango mkubwa wa mbele wa kutokea na kuwasha moto kwa lengo la kuunguza nyumba hiyo na yeye mwenyewe.
 
Kamanda huyo wa Polisi amesema watu hao pia waliunguza mlango wa nyuma eneo la jikoni katika chumba ambacho kwa kawaida mwalimu huyo huifadhia pikipiki na jenereta  lakini bahati nzuri siku hiyo vitu hivyo vilihifadhiwa sebuleni.
 
Mwakyoma amesema watu hao waliamini kuwa wakichoma vitu hivyo basi moja kwa moja vingesababisha mlipuko mkubwa kutokana na petroli iliyokuwa kwenye matanki ya pikipiki na jenereta hivyo mwalimu huyo na nyumba yake  ingeteketea kwa moto lakini kutokana na kuwa havikuwepo ni vitu vichache tu viliungua
 
Ametaja Vitu vilivyoungua katika eneo hilo la jikoni ni nyavu za dirishani na vyombo kidogo vya jikoni na kwa upande wa mlango wa mbele ya nyumba wahalifu walipanga viti na kuweka nyasi na kuchoma ambapo nyasi ziliungua na viti kidogo lakini mlango haukupata madhara makubwa
 
Mwakyoma amesema kutokana na uchunguzi wa awali ulibaini kuwa mwalimu mkuu huyo analalamikiwa kwamba alitumia lugha inayoonekana ni kashfa kwa dini ya Kiislamu hivyo kuamsha hasira kwa wazazi na ikasambaa kwenye vijiji vingine vitatu wilayani humo.
 
Kamanda huyo wa Polisi Pwani alisema kutokana na tukio la kuchomewa moto na taarifa za awali zilizopatikana kwenye uchunguzi   taarifa ziliufikia Uongozi wa Wilaya ya Kisarawe ambapo baada ya tukio hilo la uchomaji nyumba Mwalimu huyo alilazimika kuhamishwa kituo cha kazi wilayani humo na hadi jana hali ya usalama ni shwari katika vijiji hivyo.
 
Mwisho.

Related posts:

Related Ways to Take Action:
Powered by Social Actions

Leave a Reply