The Sound Of Africa
Saturday May 19th 2012

Interesting Sites

Insider

Archives

Kiongozi wa dini awatahadhalisha wanasiasa.

Na Philipo Lulale, Mtwara.

 
Kiongozi mmoja wa kanisa amewataka viongozi wa serikali kuwa wangalifu wakati wanapotoa ufafanuzi na matamshi kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazokabili taifa ili kuhakikisha kauli zao hazihatarishi amani,umoja na mshikamano wa taifa.
Hatua hiyo imeelezwa itasaidia sana kudumisha amani ya nchi na hivyo kuwa rahisi  kuendeleza hali ya mshikamano na kuwepo
uhuru wa kuabudu kwa amani na utulivu ambao kila raia wa Tanzania anauhitaji.
 
Mwenyekiti wa umoja wa makanisa ya kikristo katika manispaa ya Mtwara mchungaji Luca Mbedule amesema hayo katika risara aliyotoa kwa niaba ya umoja huo kwenye ibada maalum ya kuombea taifa iliyofanyika jana katika uwanja wa umoja mjini Mtwara.
 
Amesema kama amani ya taifa ikipotea watakaoathirika ni watanazania wote bila kujali itikadi,dini,hali wala kabila la mtu ambapo amesisitiza kuwa katika kipindi hiki taifa linapoingia katika vuguvugu la mabadiliko ya siasa,katiba na changamoto mbalimbali zinazozua mijadala mikubwa umakini kabla ya kusema chchote ni muhimu sana kwa mstabali wa taifa.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mtwara bw. Elaston Mbwilo katika salam zake kwa niaba ya serikali amewataka viongozi wa
madhehebu kuelimisha waumini wao juu ya maswala mbalimbali yanayotokea katika taifa ikiwemo kuwajengea ufahamu juu umuhimu
wa kuzingatia sheria na taratibu za nchi ili kudumisha amani na mshikamano wa taifa.
 
Aidha amewataka viongozi wa makanisa katika manispaa ya Mtwara kuhakikisha yanadumisha umoja huo ambao utasaidia sana walengwa
katika mambo mbalimbali ikiwemo maswala ya kidini na yale ya kijamii kwani hatua hiyo inaimarisha mshikamano na amani katika jamii. 
 
Ibada hiyo ya maombi maalum ililenga pamoja na mambo mengine kumshukuru Mungu kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2010,kumwomba
kuliepusha  taifa na siasa za jazba zinazoweza kuhatarisha amani ya nchi,kumwombea Rais, serikali na viongozi ili waweze kuendesha maswala
muhimu kama mabadiliko ya katiba na changamoto kama dowons na maslahi ya umma kwa hekima.
MWISHO

Related posts:

Related Ways to Take Action:
Powered by Social Actions

Leave a Reply